Kuliko LTD


MAELEKEZO

Kuliko Ltd ni biashara ya kijamii mjini Tegeta, Dar es Salaam, ambayo lengo lake la msingi ni afya ya umma kwa kutumia mfumo wa kujitegemea, mfano wa biashara ya kawaida, madhumuni ya Kuliko ni kufikia athari za kijamii kwa kiwango kikubwa kwa ushirikiano wa karibu na taasisi ya afya binafsi na ya umma, mashirika yasiyo ya faida na kupitia mtandao wa wadhamini wa afya.

MATOKEO YA KIJAMII

1. Kazi yetu sisi ni kuhakikisha afya ya mama anayejifungua, afya ya mtoto mchanga, na usalama wa kazi ya wakunga, yote katika hatari ya kukumbwa na magonjwa. Kupitia elimu na habar, tunatoa zana katika njia rahisi, na hali ya kuridhisha katika maeneo ambayo yana uhitaji zaidi . Kwa njia hii tunasaidia kupunguza kiwango cha vifo vya watoto wachanga.

2. Tunawawezesha single mothers na wajane kwa kuendesha biashara kwa mafanikio katika mfumo wa social franchise, kuwapatia mafunzo, misaada ya kifedha na zana nyingine zozote, ili katika jamii waje kua wadhamini wa afya.

Kuliko Ltd inafanya kazi kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, NGOs duniani kote, taasisi za fedha, makampuni ya mikopo midogo midogo, makampuni mengine ya kijamii, mitandao ya wajasiriamali, na Ubalozi wa Tanzania nchini Italia.

ujauzito

SHUGHULI TUNAZOFANYA

Kampuni ya kuliko imezaliwa kwa lengo la kuleta maendeleo ya jamii kwa muundo wa biashara (social enterprise).Kampuni hii ni ya kujitegemea isiyo na wafadhili kutoka nje ya nchi.

1. HOSPITALI

Tunatafuta hospitali kubwa na ndogo,tunaanza ushirikiano (kuzingatia uaminifu na kujituma). Tunasaidia hospitali kutatua matatizo/mahitaji ambayo ni;

a.Kukosa vifaa vya kujifungulia.
b.Mama wajawazito kutojua kuhusu vifaa vya kujifungulia.
c.Hatari ya mkunga kupata magonjwa.
d.Hatari ya mama na mtoto kupata magonjwa au vifo.

Kutokana na matatizo hayo,kampuni ya kuliko kwa ushirikiano na hospitali tunatoa elimu kwa kina mama wajawazito kuhusu kujifungua na kulinda watoto wachanga.

2. HEALTH PROMOTERS

Tunatafuta kina mama bora (ambao wana elimu kidogo kuhusu afya na waaminifu),tunawapa elimu na kwenda nao hospitali mpaka wanapoweza kufanya kazi wenyewe.Tunafanya hivi kama mashirika mengine yasiyo ya kiserikali (NGOs) na social franchising organization.

3. VIFAA VYA KUJIFUNGULIA (MAMA KIT)

Mama kit ni pakeji ambayo ina vifaa vyote vya kujifungulia vinavyonunuliwa ndani ya Tanzania kutoka kwa wasambazaji bora na famasia.Tunaangalia vifaa kwa umakini kwa kuangalia ubora (quality control) na kuvipaki kiubora. Muhimu sana: hakuna dawa ndani ya mama kit.

4. ELIMU

Tunatoa elimu kwa kina mama wajawazito kuhusu kujifungua salama na kutunza watoto wadogo kwa kutumia semina,DVD,vipeperushi nk.

5. USHIRIKIANO NA MASHIRIKA BINAFSI YASIYO YAKISERIKALI

Tunashirikiana pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali, saccos na mashirika mengine yaliyopo Tanzania na Ulaya.


3 thoughts on “Kuliko LTD

Comments are closed.